0
Mh Davis Mosha akiwa na Mwenyekiti wa KDFAA Ndugu Msasu.




Mgombea Ubunge wa Moshi Mjini kupitia Tiketi ya ccm Mh. Davis Mosha Amekutana na wasanii wa Filamu, Maigizo ya Jukwaani, Sarakasi na Muziki wa Mjini moshi. Wasanii hao wakiongozwa na Chama cha Wigizaji na wacheza filam Kilimanjaro (KDFAA)
Wasanii wakimsikiliza Mh. Davis Mosha wakati akizungumza nao Leo jioni.


Wasanii hao walioomba Mkutano na Mh. Davis Mosha leo katika ukumbi wa ccm Mkoa walipata fursa ya kuzungumza Changamoto zinazowakabili na Malengo yao kama wasanii wa Moshi na Mkoa Kilimanjaro. Wakiongea kwa nyakati tofauti katika ukumbu huo mmoja wa Wasanii wa Muziki Ndugu Samwel Stephen aliweza kumuomba Mh. Davis Mosha awasaidie kupata studio ya kisasa na kuwapa wigo mpana wa kazi zao za muziki kuweza kupigwa katika Radio.

Mh. Davis Mosha akijibu hilo aliwahakikishia Kujenga Studio ya Kisasa itakayoanza kufanya kazi mapema Mwezi ujao chini ya Kampuni yake ya African Swahili Media sambamba na Kufungua kituo cha Redio na Tv.

Wasanii wa Filamu waliomba kuweza kusaidiwa kurekodi Tamthilia ambayo itaweza kurushwa katika Tv na waweze kujitangaza na kujiajiri kupitia sanaa hiyo lakini pia hawakusita kutoa kilio chao juu ya Wizi wa kazi zao unaofanywa na wasambazaji pamoja na Wasambazaji kutoka Dar es Salaam kuwanyonya na kusababisha kazi zao za Film kubaki nyumbani badala ya kwenda Sokoni. Pia waliweza kutoa malalamiko yao juu ya uongozi uliokuwepo madarakani katika ngazi ya ubunge na Udiwani kuwaahidi maramara ahadi ambazo hazitekelezeki.
Mh Davis Mosha akifafanua Jambo katika Mkutano na Wasanii Leo

Bwana Mosha aliweza kuwahakikishia Soko la uhakika la filam zao na pia ulinzi wa kazi zao kupitia vyombo husika vinavyoshughulikia masuala ya haki miliki na pia kuweza kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao. Na pia aligusia suala la wasanii wa Ngoma za asili juu ya kuhakikisha anaweka kituo cha sanaa na utalii ili kuweza kuwakutanisha wageni wanaokuja kupanda mlima na kufanya ni kituo cha kubuudika kupitia ngoma za asili na sehemu ya kujifunzi aTamaduni za Makabila mbalimbali ya Tanzania. LAkini pia aliwaasa wasanii kutumia sanaa yao kutoa elimu ya uchaguzi juu ya wananchi kutumia haki yao ya msingi katika kuchagua na wasifanye makosa watumie Mitaji yao ya Vitambulisho vya kupigia kura kuhakikisha wanachagua Kiongozi atakayeenda kufanya kazi na si mwanasiasa.


Mwenyekiti wa KDFAA akitoa shukrani zake kw Mh. Davis Mosha kwa Kukubali kuja kuwasikiliza.


 Akifunga Mkutano huo wa wasanii, Mwenyekiti wa Chama cha waigizaji na Filamu Ndugu Msasu alitoa shukrani za Dhati kwa Mh. Davis Mosha huku akimfananisha na Mkombozi ambaye amekuja kuwakomboa kutokana na Viongozi wengi kuwadharau wasaniii na kupelekea Sanaa ya Moshi kuzidi kushuka. Alitumia nafasi hiyo kuwaasa wasanii kutochezea nafasi waliyopata ambayo Mh. Davis Mosha ameonesha nia ya dhati ya kuweza kuwakomboa kupitia sanaa yao na wao basi waoneshe hitaji lao kwake kwa kuhakikisha wanafanya kazi nzuri katika sanaa.

Post a Comment

 
Top