0



Polisi wakiwasambaratisha vijana wanaosadikiwa wa Chadema huku vijana hao wakiwatrushia polisi Mawe.
Vijana wanaosadikiwa kuwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleov Chadema  wamevunja Mkutano wa Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi jimbo la Moshi Mjini Mh. Davis Elisa Mosha.  Tukio hilo limetokea leo katika kata ya Rau mtaa wa rau Madukani.
Jeshi la Polisi wakiwa wamemtia nguvuni baadhi ya vijana waliokua wakileta fujo.



Katika tukio hilo Mh. Davis Mosha alikua na Mkutano wa kampeni katika kata hiyo ya Rau ndipo maandalizi ya mkutano huo yakaanza mapema Asubuhi. Ilipofika muda wa saa tano Asubuhi lilikuja kundi kubwa la vijana wanaosadikiwa wafuasi wa Chadema na kuanza kufunga bendera za chadema katika eneo hilo ambalo ccm walikua wakifanya mkutano. Baada ya bendera hizo kufungwa ndipo wanachama na viongozi wa ccm walipokuja na kutaka kutoa bendera hizo lakini vijana hao walioonekana kupangwa kwa ajili ya tukio hilo walipotishia iwapo bendera hizo zitashushwa basi damu itamwagika. Kutokana na kauli hiyo huku vijana hao wakiwa wamekusanya mawe sehemu moja ililazimu viongozi hao kuwasiliana na jeshi la polisi ili kuweza kusimamia amani katika eneo hilo.


Mmoja wa Mwanachama wa ccm akiomba msaada baada ya kujeruhiwa kwa jiwe.

Baada ya polisi kuwasili pamoja na kikosi cha kutuliza ghasia vijana hao walianza kurusha mawe kushambulia jeshi la polisi pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi waliopo katika eneo hilo. Katika mashambulizi hayo yaliweza kujeruhi wanachama wa ccm na raia kadhaa waliokua katika eneo hilo. Jeshi la Polisi liliweza kumkamata kijana aliyefahamika kwa jina la  Remy ambaye ndiye anayesadikiwa kuongoza kundi hilo la vijana wanaokadiriwa kufika sitini. Kiongozi huyo wa kundi hilo amekamatwa pamoja na wenzake wane huku wengine wakitokomea kusikojulikana.

Kiongozi  wa kundi la vijana ambao  hao mwenye kilemba akitoa maelekezo kwa vijana hao.



Davis Mosha aliweza kuzungumza kuhusu tukio hilo alisisitiza wananchi wa Moshi kuilinda amani ya Moshi na kuwaasa vijana kuepuka na kundi dogo la watu ambao wana maslahi binafsi na kuwatumia katika uvunjwaji wa amani. Vurugu hizo zimepelekea mkutano huo kuvunjika.  


Kijana aliyetambulika kwa jina la Remy ambaye ndiye kiongozi wa kundi lililoleta fujo katika mkutano.

Jeshi la polisi likiwa limewakamata baadhi ya vijana ambao walikua wakileta vurugu katika mkutano wa ccm.

Post a Comment

 
Top