0


Ikiwa ni siku chache tu tokkipenga cha kampeni za kuwania nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani Kupulizwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wagombea mbalimbali wameanza kampeni za kuomba kura katika majimbo yao. Kwa upande wa Moshi mjini ambapo ni jimbo ambalo limeongozwa na upinzani kwa muda mrefu sasa hali ya kisiasa imebadilika.
Mh. Davis Mosha Akiwasalimu wananchi wa Moshi

Wananchi mbalimbali wameonekana kuchoshwa na ahadi zilizokua zikitolewa mara kwa mara na upinzani na ahadi hizo hazijatekelezwa. Ujio wa Mgombea ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mh. Davis Elisa Mosha umeonekana kama ni ukombozi kwa wakazi wa Moshi. Hilo lilijidhihirisha Juzi katika mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia tiketi ya ccm Bi. Samiah Suluhu uliofanyika katika viwanja vya ccm kata ya majengo baada ya Mh. Davis Mosha kuwasili katika mkutano dakika chache baada ya Mkutano kuanza na kujikuta akipokewa kwa shangwe na nderemo huku kila mtu akihitaji kumshika mkono na wengine hata kupiga nae picha za kumbukumbu.

Mh. Davis Mosha akipokewa na wananchi baada ya kuwasili kwenye Mkutano







Mh. Davis Mosha alipewa dakika moja ya kusalimia ambapo wananchi walilipuka kwa furaha huku wakiimba nyimbo za tumaini jipya la maendeleo ndani ya Mji wa Moshi. Hali hiyo iliamsha hisia kubwa kwa Chama cha mapinduzi na kujivunia kwa kuchagua mtu sahihi wa kulikomboa Jimbo.

Mh. Davis Mosha akiwasalimu wananchi wa Moshi alipokua akiwasili katika mkutano.


Mwandishi wetu alizungumza na watu mbalimbali na walieleza imani kubwa walio nayo juu ya Mh. Davis Mosha na kushukuru kwa kuona wakati huu ndio sahihi wa kurudi nyumbani na kuwatumikia wananchi wa Moshi mjini. Akijibu swali la Muandishi ndugu Erasto Mushi wa Bomambuzi juu ya baadhi ya watu kusema Mh. Davis Mosha aishi Moshi, Erasto alisema kwa kawaida Baba huwa anatoka nyumbani na kwenda kutafuta na anapopata basi huleta nyumbani na kujumuika na familia. Kwahiyo Davis Alikua Dar kwa ajili ya kutafuta na sasa karudi nyumbani katika mji ambao amezaliwa na kukua ili kuweza kuendeleza na anaamini kuwa Mh. Davis nafsi imemsuta kuona ndani ya Mji aliozaliwa hakuna maendeleo na uwezo wa kuyaleta upon a muda wenyewe ni huu. Alima;iza kwa kusema Wananchi wasisikilize Propaganda za kumkatisha Tamaa Davis Mosha na inapaswa kumuamini kwani Mungu kaamua kumleta mtu wake na ni vema kuhakikisha hatupotezi bahati hii.

Mh. Davis Mosha akisalimiana na Mgombea mwenza wa Urais Bi Samia Suluhu.


Ikumbukwe uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba ambapo wewe mpiga kura unakumbushwa kujitokeza kupiga kura kwa kiongozi ambaye atakuletea maendeleo na sio mwenye maneno mengi. 



Kwa jimbo la Moshi Davis Elisa Mosha anatosha.


Post a Comment

 
Top