0


Mh. Davis Mosha akiwafafanulia Jambo waandishi wa Habari.


 Huku hali ya kisiasa ikizidi kushika kasi katika Majimbo mbalimbali ya Uchaguzi Ndani ya Jimbo la Moshi hali ya siasa inazidi kushika kasi huku wagombea wa chadema na ccm wakionekana kuwa na upinzani Mkubwa ndani ya Jimbo la Moshi.

Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Moshi mjini M\Ndugu Mwita akizungumza na Waandishi wa habari.



 Akizungumza na Waandishi wa habari leo katika ofisi za ccm wilaya ya Moshi Mjini Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya ccm Ndugu Davis Mosha alisema Wananchi wa Moshi wanahitaji Maendeleo ba wanahitsji kiongozi ambaye anaweza kuwaletea mabadiliko. "Huu si Muda wa Propaganda na kuwaaminisha wananchi habari za uongo na Kutengeneza. Naomba mdahalo wa wazi na Jafari Michael ambao utatoa fursa kwa wananchi kuuliza Maswali na pia kila mmoja wetu kunadi sers na mikakati ya kuleta maendeleo ya Moshi" Alisema Davis Mosha.

Mh. Davis Mosha akijibu moja ya swali aliloulizwa na waandishi wa habari.


 Hata hivyo aliweza kuzungumzia sakata la vijana wanaosadikiwa kupigwa wakati msafara wake ukitoka katika Mkutano Pasua. Davis aliweka wazi kuwa ule ulikua ni mpango na waliujua mapema na waliitaarifu Polisi juu ya Mpango huo nia yao ikiwa ni kutafuta kura za huruma na walitaka vijana hao walale polisi ili waeneze chuki. Baada ya kujua hilo Davis alienda na kuomba wadhaminiwe hata hivyo viongozi wa chadema hakuna aliyejitokeza kuwadhamini mpaka mwanachama wa ccm alipojitosa na kuwadhamini. Kijana Said ambaye alikua mmoja wa Wahanga wa Tatizo hilo alisema yeye aliambiwa azomee msafara huo bila kufikiri Madhara yake na amejifunza kuwa amani ni kitu Muhimu. 

Baadhi ya vijana wanaosadikiwa kushambulia msafara wa Davis Mosha wakiongea na wana habari.

Post a Comment

 
Top