0

Mgombea Ubunge Moshi Mjini Davis Elisa Mosha




Mgombea ubunge Kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Jimbo la Moshi Mjini. Mh Davis Elisa Mosha amezidi kuonesha ushupavu wake katika uongozi na jinsi alivyo na hari ya kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa Moshi Mjini. Hilo limejionesha tokea kipenga cha kampeni za uchaguzi kilipopulizwa na kuanza kutaka kujua kero mbalimbali za wananchi kwa kutembelea maeneo husika.
Davis akitumia aina ambayo inawachanganya wapinzani wake na bila kujua atakuwa wapi amekua akitokeza katika maeneo mbalimbali bila taarifa na kuzungumza na wakazi wa eneo hilo huku akitazama changamoto zao na kuweka mikakati ya kuzifanyia kazi. Akiwa katika Soko la Mbuyuni Mapema wiki hii Davis alizungumza na wakina mama wafanyabishara wa soko hilo na klupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuwaahidi kuzifanyia kazi mapema.
“Natamani ningeanza kazi Sasa hivi kuondoa hizi kero na kinachonishangaza kwanini mnaishi katika soko ambalo mnalipia mapato lakini hakuna Maji safi na salama” Davis aliwaambia wafanyabiashara wa Soko la Manyema.
Ikiwa Kampeni zinazidi kushika kasi ndani ya jimbo hilo Davis Elisa Mosha amefanya mikutano kadhaa na kuweza kuzungumza na wananchi juu ya maendeleo ya Jombo la Moshi.  “Huyu kijana ni kiongozi kweli na ana nia ya dhati si wakati wa kupoteza watu kama hawa katika mji wetu wa Moshi ni wakati wa kumchagua na kushirikiana nae” Alisema Christina Minja Mfanyabiashara wa chakula eneo la Shabaha Moshi.

Tazama Picha zaidi......,


Mh. Davis Mosha akiwa na Wazee wa Baraza la wazee ccm


Mh. Davis Mosha akiagana na wazee wa ccm baada ya picha ya pamoja.

Wananchi na wafanyabiashara ndogondogo wa eneo la Shabaha Moshi mjini wakifurahi pamoja na Mh. Davis Mosha


Mh. Davis Mosha akizindua Shina la wakereketwa wa Soweto MASKANI YA KIKWETE
Mh. Davis Mosha akizungumza na wakazi wa Kata ya Soweto.

Mh. Davis Mosha akiwanadi wagombea udiwani wa kata ya Soweto, Karanga na Shirimatunda

Wananchi wa Moshi mjini wakiwa katika Moja ya Mikutano ya Kampeni za Mh. Davis Mosha

Mh. Davis Mosha akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Manyema.

Mh. Davis Mosha akisalimiana na Mfanyabiashara ndogondogo wa soko la Mbuyuni baada ya kuzungumza nao alipowakuta wakipata chakula mchana.  

Mh Davis Mosha akisalimia alipopita katika kampeni za Mgombea Udiwani wa Korongoni.














Mh. Davis Mosha akiondoka katika baada ya Mkutano wa Kampeni wa Soweto

Post a Comment

 
Top