0


Mgombea Ubunge kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi ndugu Davis elisa Mosha amezindua Kampeni za Ubunge Leo kwa kishindo. Mkutano huo ulioanza leo mapema saa nane na nusu katika uwanja wa Mashujaa. Wananchi na wanachama wa ccm walionekana mapema wakiwasili katika viwanja hivyo huku wakiwa wamevalia sare za ccm sambamba na vikundi vya Hamasa walianza kuhamasisha katika Uzinduzi huo.
Mh. Davis Mosha akipiga ngoma ya Kichaga kabila lao la Wa Old Moshi alipoingia katika uwanja wa Mashujaa.

Mkutano huo mkubwa uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo katibu mkuu wa ccm Komredi Kinana, Aliyekua Mbunge wa simanjiro na mgombea ubunge wa jimbo hilo Ndugu Ole Sendeka pamoja na Mh. Lusinde maarufu kama Kibajaji.
\
Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Moshi Bi Elizabeth Minde akifungua Mkutano wa Uzinduzi wa Ubunge Leo.




Mamia ya Wananchi na wanachama wa CCM Moshi Mjini wakimsikiliza Bi. Elizabeth Minde wakati akifungua Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Ubunge

Akizungumza na wakazi wa Moshi Mh. Lusinde aliweza kutoa Tahadhari kwa wakazi wa Moshi juu ya kuendesha siasa za kashabiki zinazopelekea kuchagua kiongozi ambaye hatokua na manufaa na Moshi huku akisisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kimewaletea Mtu sahihi ambaye ni Davis Elisa Mosha. Pia Ole 
Sendeka aliweza kuwakumbusha wakazi wa Moshi juu ya Wagombea ambao wanataka kujaribu na wakiwa hawana nafasi ya kuzungumza na serikana na kuwaasa kuwa Davis Mosha ni Chaguo Sahihi kwani ni kijana mwenye mafanikio makubwa na mafanikio hayo yameletwa na juhudi na Uchapakazi alionao.

Lusinde akizungumza na Wananchi wa Moshi Leo katika Uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Moshi Mjini.


Ole Sendeka akimwaga Sera za ccm mbele ya Mamia ya wananchi wa Moshi Mjini
Baada ya Viongozi hao kuzungumza Alifuata katibu mkuu Kinana aliweza kumuelezea Ndugu Davis Elisa Mosha kama Chaguo sahihi la Magufuli huku akitoa Salamu za Mgombea Urais kupitia Tiketi ya CCM aliyeagiza kuwa wakazi wa Moshi wamchague Davis Elisa Mosha ili afanye nae kazi ya kuijenga Moshi na Tanzania kwa Ujumla.

Katibu Mkuu wa ccm Mh. Kinana akisalimia Wananchi wa Moshi mjini Pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi.

Mh. Kinana Akimnadi Mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm Mh. Davis Elisa Mosha.
Katika hali isiyotegemewa na ambayo haijawahi kutokea huku watu mbalimbali wakiifananisha hali hiyo na hali iliyotokea mwaka tisini na Tano wakati  Mrema akigombea Urais kupitia tiketi ya NCCR MAgeuzi. Sababu ya kusemwa yote hayo ni Pale Kinana Alipomuiita Davis Mosha aje azungumze na wananchi Zililipuka shangwe na furaha kwa wakazi hao wa Moshi huku wengine wakishindwa kuzuia Furaha zao na kujikuta wanatokwa na Machozi. 

davis elisa Mosha akizungumza na wananchi wa Moshi mjini Leo

Davis Elisa Mosha alitumia Takribani dakika sita kuwatuliza wananchi watulie na kumsikiliza ili azungumze nao juu ya kuijenga Moshi Mpya.  Katika Hotuba yake iliyodumu kwa dakika ishirini kutokana na Muda aliweza kuzungumzia Mambo Mbalimbali ikiwemo Afya, Ajira, Uchumi na Michezo. Ikumbukwe Davis Mosha aliweza kushinda kwa kura zaidi ya elfu nne katika kura za Maoni huku aliyemfuata akiwa na idadi ya kura Takribani mia saba tu.
Mh. Davis Elisa Mosha akimtambulisha mke Madame Nance kwa wananchi wa Moshi. 



Mamia ya wakazi wa Moshi wakimsikiliza Mgombea ubunge wa Moshi Mjini Kwa tiketi ya ccm Mh. Davis elisa Mosha

Mh. Davis Mosha wakati akifurahi na Wananchi wa Moshi Mjini.                          

Post a Comment

 
Top