MH. Mwita Mchumi wa ccm Wilaya ya Moshi mjini na Meneja Kampeni wa Mgombea Ubunge wa Moshi Mjini akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya njoro. |
Mgombea ubung kupitia
Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Mjini Mh. Davis Elisa Mosha Amwambia
Mbunge Mstaafu wa Moshi Mjini kupitia Tiketi ya Chadema Mh. Philemon Ndesamburo
awaambie wanachama wa chama hicho ukweli kuhusu Utendaji kazi wake.
Mh. Davis Elisa Mosha akisisitiza jambo kwa Mamia ya wakazi wa kata ya njoro |
Mh Davis Mosha ameyasema hayo leo katika Ufunguzi wa Kampeni
za Udiwani katika kata ya Njoro, Mh. Davis Mosha akizungumza na Umati wa
wananchi wa Kata hiyo ya Njoro alisema Anamuheshimu sana Mzee Ndesamburo ka
Kazi aliyoifanya katika kipindi alichokua na Hana shaka katika hilo na anajua
fika Mzee Ndesamburo anajua Utendaji wake wa Kazi.”Mzee Ndesamburo anajua mimi
ni Mpambanaji, na anajua fika kuwa mimi ndiye iongozi sahihi ninayeweza
kuwavusha kutoka hapa alipowaanha mpaka kwnye maendeleo. Nawatuma nendeni
kamwambieni kuwa asikae kimya kama ana mapenzi ya dhati na Moshi mjini basi
awaambie kuhusu mimi na afute kauli ya kurithisha jimbo kwa mtu ambaye anaamini
bado hana uwezo wa kuliongoza hili Jimbo.” Alisema Mh. Davis Mosha huku
akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi.
Mh. Davis Mosha Akiwapa nafasi wananchi wa Njoro kusema changamoto zinazowakabili. |
Hata hivyo Mh. Davis Mosha hakuacha kueleza wananchi juu ya
utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa moshi ikiwemo Ajira
kwa vijana, Afya, Elimu na Hali ya Ulinzi na Usalama wa Moshi. Davis Mosha
aliwaambia wakazi wa Njoro kumchagua kwa kishindo Diwani wa Kata hiyo Ndugu Zuberi
na kuongeza kuwa ni mchapakazi na ataweza kufanya nae kazi kwa usahihi. Pia
aliwaomba kuhamasisha ndugu zao na wakazi wa kata mbalimbali kuwachagua
madiwani wa Chama cha Mapinduzi na katika kura ya Urais Mh. Magufuli anatosha
na katika Ubunge hapo si pakufanya makosa ni Davis elisa Mosha.
Mkutano huo uliisha ka maandamano makubwa yaliyokua
yakimsindikiza Mh. Davis Mosha wakati anatoka katika viwanja vya Relway eneo
ambalo ulifanyika mkutano huo.
Mamia ya wakazi wa Moshi wakimsikiliza Mgombea Ubunge Moshi mjini Mh. Davis Mosha |
Mh. Davis Mosha akinadi Sera za chama cha Mapinduzi kwa wananchi wa Njoro |
Mgombea Udiwani kata ya Njoro Mh. Zuberi akitoa salamu ya ccm kwa wakazi wa Njoro. |
Wananchi wa Njoro wakiwa wamembeba Mh. Davis Mosha baada ya Kuisha kwa Mkutano |
Umati wa wakazi wa Njoro ukisindikiza Gari alilopanda Mh. Davis Mosha baada ya Mkutano kumalizika. |
Post a Comment