0

helkopta  iliyombeba mgombea Ubunge wa Moshi Mjini Mh. Davis Mosha ikiwa angani kabla ya kutua uwanja wa mashujaa katika mkutano wake wa kwanza wa Kampeni 

Mgombea ubunge kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ndani ya Jimbo la Moshi Mjini Ndugu Davis Elisa Mosha azidi kuwachanganya Chadema ndani ya Jimbo la Moshi. Hali hiyo imezidi kujidhihirisha baada ya Mgombea huyo kufanya mikutano miwili tu mpaka sasa na kubadili hali ya hewa katika jimbo la Moshi.

Maelfu ya wakazi wa Moshi wakimpokea Mgombea ubunge Mh. davis Elisa mosha wakati akiingia  katika mkutano wa kwanza wa kampeni za ubunge wa Moshi mjini.


Ikiwa inafahamika Jimbo la Moshi ni Ngome kuu ya upinzani tokea uchaguzi huru wa vyama vingi uanze mwaka 1995 mpaka sasa jimbo hilo linaongozwa na Upinzani. Ujio wa Davis Mosha kugombea ubunge kupitia ccm umewachanganya wapinzani huku wakishindwa kunadi sera na kujikita kuzungumzia maisha binafsi ya Davis Mosha. Mmoja wa Makada wa Chadema ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Mosha amefanya kazi imekua ngumu na si kama tulivyomtarajia, Sasa tunafanyavikao kila dakika, Magari ya matangazo yanafanya kazi mpaka nyakati za usiku. Huyu bwana anakubalika sana, Kiukweli hali ya chama chetu ndani ya Jimbo la Moshi ni Mbaya" Alimaliza kusema kada huyo.

Mh. Davis Mosha akizungumza na wananchi wa Moshi


Mh. Davis Elisa Mosha akimkaribisha mwanachama mpya wa ccm

Tulipomtafuta Davis Mosha na kuzungumza nae kuhusu mikakati yake ya kuhusu Mchakato wa Uchaguzi alisema yeye amekuja kuleta maendeleo Moshi na hajaja kusikiliza wakatisha tamaa na wanaotaka madaraka kwa ajili ya Faida zao binafsi. Anajua anadeni kubwa kwa watu wa Moshi, Yeye aliondoka Moshi na kwenda kutafuta baada ya kuona familia yake inahitaji maisha mazuri na yeye kama mmoja wa watoto wa kiume katika familia yake ilimbidi aende Dar es Salaam kutafuta na dua za wazazi wake zilitimia akapata na sasa amerudi kuhakikisha anaujenga mji wake na mji wa wazazi wake na mji ambao ni kitovu chake. Mji wa Moshi unaidai, Unanidai fadhila ambazo wakazi wake wameonesha kwa wazazi wangu, Sasa na mimi ni lazima nirudishe fadhila zangu kwa wakazi wa Moshi, Moshi haina Hospitali ya wilaya, Moshi haina Eneo maalumu kwa ajili ya Michezo, Mahospitalini hakuna Mfumo mzuri wa utunzwaji wa dawa na kupelekea Dawa kuharibika na nyingine kuisha haraka, Vijana wa Moshi hawana Ajira wanahitaji kuwezeshwa na kutengenezewa mfumo sahihi wa kujiajiri. Huu si wakati wa kulumbana majukwaani na kutoleana matusi. Huu ni wakati wa kuwaeleza wananchi wa Moshi unatarajia kuwafanyia nini. Mimi sina cha kusema kwa sasa kuwa nimefanya kwa mji wa Moshi kile nilichofanya nilifanya kama Davis Mosha na sio Mbunge wala Diwani. Ila kuna watu wameshika uongozi ni miaka kumi sasa wawaambie watu wa Moshi ni niniwamewafanyia sio kuwaambia watu wa Moshi kuwa Davis anaishi dar. Hiyo inamaanisha kuwa wachaga wote waliopo mikoani wasirudi kwao na kuwekeza sababu biashara zao hazipo Moshi" Alimaliza kuzungumza.
Wananchi wa Njoro wakimsikiliza mgombea ubunge wa Moshi mjini mh. Davis Elisa Mosha



Mh. Davis Mosha pamoja nMgombea udiwani wa kata ya njoro wakiwa wamebebwa na wananchi wa kata hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano wake wapili wa kampeni
 
Davis Mosha anatarajia kufanya mkutano wa Tatu siku ya Jumamosi ya tarehe 12/09/2015 katika kata ya kiboriloni na atazungumza na wakazi wa kata  hiyo huku akiwaomba wakazi wa kata ya Kiboriloni ambayo ndio nyumbani kwao wajitokeze kwa wingi na kumsikiliza ni nini atawafanyia na si kuja kujibu hoja za wapinzani wake. 
Mh. Davis Elisa Mosha akiwaaga wananchi wa njoro waliojikusanya pembezoni mwa barabara wakati anaondoka katika mkutano.



Post a Comment

 
Top