3

Gaga akizungumza na wakazi wa Kata ya Kiboriloni



Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapindizi Ndugu Davis Elisa Mosha ameshangazwa na Kauli za Aliyekua Mbunge wa Moshi Mjini Mzee Philemon Ndesamburo. Davis Mosha alisema hayo jana katika Mkutano wake wa Tatu wa Kampeni tokea Kampeni zifunguliwe rasmi. Davis Mosha alisema anashangazwa na kauli za ndesamburo zinazoashiria kuwa hamfahamu wakati ni mmoja wa watu wake wa Karia sana na wanaheshimiana sana. "Sikutegemea Ndesamburo kupanda Jukwaani na kunizungumzia ikiwa mimi na yeye hatuna ugomvi wala hakuna mahali tumewahi kukwazana na mimi kuja kugombea hapa Moshi tayari nilipokea Baraka zake. Leo akisema hanijui basi atakua anadanganya wananchi wa Moshi. Akija hapa kwa mara nyingine mwambieni awaambie Ukweli.

Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Mh. Agrey Mareale akizungumza na Wananchi wa Kiboriloni


Pia Mgombea huyo alizungumzia malalamiko ya Mzee Ndesamburo anayomtuhumu kumny'ang'anya wafanyakazi wake wawili ambao ni John Maarufu kama Laperee na mwingine aliyefahamika kwa jina Moja tu la Gaga. Mosha alisema ndesamburo anajua fika kwanini hawa vijana wapo kwangu na wananifanyia kampeni sasa kwanini leo apande jukwaani na kuwakana wakati tayari kuna makubaliano. Davis alikata mzizi wa fitina na kuwaita Jukwaani Gaga na Laperee na kuwapa nfasi wazungumze kwanini wapo na Davis na sio Jafari.


Mamia ya wananchi wa kiboriloni wakimsikiliza Mh. Davis Mosha

Akiongea na Umati mkubwa wa Wananchi wa Kiboriloni Gaga alionesha ujumbe wa maneno katika simu yake ambao ulisomwa na mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano huo ujumbe ambao ulikua ukimuita Gaga aonane na Ndesamburo na ujumbe huo ulitoka kwa Ndesamburo. Gaga alisema yeye alitii wito wa bosi wake na kufika kwa Ndesamburo na akamkuta Davis Mosha na Ndesamburo baada ya Muda akaingia Laperee na kuanza Mazungumzo. Gaga alizidi kuongea akisema Mzee aliwatambulisha kwa Davis na kuwapa kazi ya kuhakikisha wanamnadi Davis mpaka anashinda ubunge na hawezi kuachia jimbo likaenda kwa mtu Chasaka (Akimaanisha Kabil tofauti na lake) na kuwaahidi kuwa yeye atakua nyuma yao na hatoweza kujionesha kwa kuwa ni kiongozi katika chama. Hivyo basi yeye na John wanafanya kazi maalumu ambayo wamepewa na Ndesamburo wananchi wasiwaone ni wasaliti wao wanatimiza kazi ya Bosi wao.



Mh. Davis Mosha akizungumza na wakazi wa kata ya Kiboriloni

Laperee nae alipata fursa ya kuzungumza alisema yeye hawezi mtukana wala kumsema vibaya Mzee Ndesamburo, Anamuheshimu na yupo ccm kwa kazi maalumu ya kuhakikisha Davis anashinda kama walivyokubaliana na anachoweza kumuahidi ni kuwa ile ahadi yake ya pale kwenye kikao ataitimiza kwa asilimia miamoja na hatomuangusha.



Hata hivyo Davis Mosha alitumia nafasi hiyo kwa kuzungumza na wananchi wa Kiboriloni kwa kuelezea vipaumbele vyake ambavyo anatarajia kuvitekeleza iwapo tu watampa ridhaa ya kuongoza jimbo la Moshi Mjini.


Post a Comment

  1. Agar ap kisi ka dil moom bnana chahtay hain ap chahtay hain ap ka teacher ap k, ap k maa bap bahn bhai, rishta dar waghera jo boht gusay walay hain ap chahtay hain k un ka dil mom ho jay or aap se pyar se bat krain or ap se kbhi na jhagray to is k liya ap abhi Shah Faisal Jaferi sb ko call krain.
    Online Istikhara
    Rohaniilaj
    Wazaif
    Nori ilam
    Taweez
    Rohani Zaicha
    Horoscope
    Astrology
    Rohaniilaj in Dubai
    Black Magic ka tor
    Amil Online
    Amiliyat
    Husband wife problems
    Marriage problem
    Istikhara for Marriage
    Istikhara

    ReplyDelete
  2. Ais masla ka hall 1 choti sa dua ma mojod ha Jub b aps afar k liya niklan to Safer ki dua Zaror Parhan InShallah Duran Safer ap Allah ki Mana ma hon ga Inshallah Dunya ki koi taka tap ko nksan ni pouncha sakti.
    Online Istikhara
    Rohaniilaj
    Wazaif
    Nori ilam
    Taweez
    Rohani Zaicha
    Horoscope
    Astrology
    Rohaniilaj in Dubai
    Black Magic ka tor
    Amil Online
    Amiliyat
    Husband wife problems
    Marriage problem

    ReplyDelete

 
Top