0

Mh. Davis Mosha akizungumza na Mamia ya wakazi wa Pasua leo


Ikiwa kampeni za Waombea Nafasi mbalimbali za Uongozi zikizidi kushika kasi katika majimbo mbalimbali, Leo Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini Mh. Davis Mosha amepasua ngome ya Mpinzani wake Mkubwa kwa tiketi ya Chadema Ndugu Jafari Michael. Ikiwa Kata ya Pasua ni moja ya kata kubwa ndani ya anispaa ya Moshi na Moja ya Ngome kuu ya Chadema na ni Eneo ambalo anatokea Mgombea huyo wa Chadema hali imekua tofauti katika Eneo Hilo baada ya Davis Mosha kufanya Mkutano mkubwa wa kampeni na Kuondoka na Mwenyekiti wa Bawacha wa kata ya Pasua pamoja na Aliyekua Mwenyekiti wa Mtaa katika kata hiyo kupitia Chadema.


Mh. DAvis Mosha Akiwapungia wakazi wa Pasua leo


Akizunumza katika mkutano huo uliokua umefurika watu Davis Mosha alituma salamu kwa mgombea huyo wa Chadema kuwa ndio kaanza kazi Rasmi ya kulikomboa jimbo na Ataeleza ukweli juu ya Mipango ya maendeleo ya Moshi na atatoa elimu kwa wakazi wa Moshi kuhusu mfumo wa uendeshwaji wa jimbo ambao hawafahamu na wamekua wakidanganya na kukosa haki zao za Msingi.


Mamia ya wananchi Pasua katika mkutano wa Kampeni za ccm leo

Pia Mjumbe wa Kamati kuu ya ccm Taifa Mh. Agrey Marealle aliwaeleza wakazi wa kata ya Pasua kufanya maamuzi sahihi katika kuchagua na Ndugu Davis Mosha ametosheka na anaenda Bungeni kuleta maendeleo si kutafuta fedha. Pia alisema majeruhi yanayoendelea kwa Jafari Michael ni sababu ya wananchi na viongozi wao kuchoshwa na mfumo mmoja wa Chadema wa kurithishana uongozi huku watu wanaoitolea katika chama na wenye uwezo wakinyimwa nafasi mpaka kufikia kushindwa kuelewa neno Demokrasia katika chama hicho. "Njooni ccm kwenye Demokrasia ya kweli" Alimaliza Mh. Agrey Marealle.



Mjumbe wa kamati kuu ya ccm Mh Agrey Marealle akizungumza na wakazi wa Pasua Leo.




Post a Comment

 
Top