0


Katika hali isiyotegemewa leo majira ya asubuhi mgombea ubunge wa jimbo la Moshi Mjini lililopo Mkoani Kilimanjaro kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Bwana Davis Mosha  asimamishwa na kundi kubwa la wananchi  wa jimbo hilo ili kueleza kero zao.
Mgombea ubunge huyo alikuwa akitokea nyumbani kwake maeneo ya Kiboroloni kuelekea ofisi ya ccm kata ya korongoni na alipofika maeneo ya kituo kikubwa cha mabasi yanayokwenda mikoani aliweza kusimamishwa na umati wa wananchi hususani vijana kwa lengo la kuweza kumueleza shida zao.
Baadhi ya wananchi walioweza kueleza shida zao ni wapiga debe pamoja na wakina mama wanaojishughulisha na biashara ya upikaji chakula maarufu kama mama lishe ambao waliweza kumueleza Bwana Davis kuwa wamekuwa wakisumbuliwa sana na Mgambo wa Manispaa kwa kuweza kuwafukuza katika maeneno yao ambayo wanayatumia kwa ajili ya kutafutia ridhiki.

Halikadhalika pia kwa wapiga bede pamoja na wafanya biashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga pia hawakuweza kuwa nyumba kumueleza Bwana Davis Mosha baadhi ya shida ambazo wanazipata pindi wanapofanya kazi zao maeneno ya stand.

“Ni kweli nafahau matatizo yenu najua ni jinsi gani mnapata shida lakini mimi napenda kuwaahidi kuwa pindi mtakaponichagua niongoze jimbo hili nawaahidi kuwa matatizo haya nitaweza kuyashughulikia na yataisha na mtafanya kazi kwa amani sana” alisema Bwana Davis Mosha


Hii sio mara ya kwanza mgombea mbunge huyu kuweza kusimamishwa na wananchi katika hali isiyotarajiwa.

Mh. Davis Mosha akimsikiliza mama anayefanya biashara ya chakula katika eneo la stand akieleza kero na adha wanazopata.

Muendesha Mkokoteni akifafanua jambo kwa Mh. Davis Mosha





Wananchi wa Moshi mjini wanaofanya kazi eneo la stand kuu ya mabasi mjini Moshi wakishangilia baada ya Mh. Davis Mosha kuzungumza nao.




Wananchi wakimfuata Mh Davis Mosha wakati akielekea ndani ya Stand kuu ya Mabasi









Post a Comment

 
Top