Ikiwa ni siku chache tu tokkipenga cha kampeni za kuwania
nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani Kupulizwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Wagombea mbalimbali wameanza kampeni za kuomba kura katika majimbo yao. Kwa
upande wa Moshi mjini ambapo ni jimbo ambalo limeongozwa na upinzani kwa muda
mrefu sasa hali ya kisiasa imebadilika.
Mh. Davis Mosha Akiwasalimu wananchi wa Moshi |
Wananchi mbalimbali wameonekana kuchoshwa na ahadi zilizokua
zikitolewa mara kwa mara na upinzani na ahadi hizo hazijatekelezwa. Ujio wa
Mgombea ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mh. Davis Elisa Mosha
umeonekana kama ni ukombozi kwa wakazi wa Moshi. Hilo lilijidhihirisha Juzi
katika mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia tiketi ya ccm Bi. Samiah
Suluhu uliofanyika katika viwanja vya ccm kata ya majengo baada ya Mh. Davis
Mosha kuwasili katika mkutano dakika chache baada ya Mkutano kuanza na kujikuta
akipokewa kwa shangwe na nderemo huku kila mtu akihitaji kumshika mkono na
wengine hata kupiga nae picha za kumbukumbu.
Mh. Davis Mosha akipokewa na wananchi baada ya kuwasili kwenye Mkutano |
Mh. Davis Mosha alipewa dakika moja ya kusalimia ambapo
wananchi walilipuka kwa furaha huku wakiimba nyimbo za tumaini jipya la
maendeleo ndani ya Mji wa Moshi. Hali hiyo iliamsha hisia kubwa kwa Chama cha
mapinduzi na kujivunia kwa kuchagua mtu sahihi wa kulikomboa Jimbo.
Mh. Davis Mosha akiwasalimu wananchi wa Moshi alipokua akiwasili katika mkutano. |
Mwandishi wetu alizungumza na watu mbalimbali na walieleza
imani kubwa walio nayo juu ya Mh. Davis Mosha na kushukuru kwa kuona wakati huu
ndio sahihi wa kurudi nyumbani na kuwatumikia wananchi wa Moshi mjini. Akijibu
swali la Muandishi ndugu Erasto Mushi wa Bomambuzi juu ya baadhi ya watu kusema
Mh. Davis Mosha aishi Moshi, Erasto alisema kwa kawaida Baba huwa anatoka
nyumbani na kwenda kutafuta na anapopata basi huleta nyumbani na kujumuika na
familia. Kwahiyo Davis Alikua Dar kwa ajili ya kutafuta na sasa karudi nyumbani
katika mji ambao amezaliwa na kukua ili kuweza kuendeleza na anaamini kuwa Mh.
Davis nafsi imemsuta kuona ndani ya Mji aliozaliwa hakuna maendeleo na uwezo wa
kuyaleta upon a muda wenyewe ni huu. Alima;iza kwa kusema Wananchi wasisikilize
Propaganda za kumkatisha Tamaa Davis Mosha na inapaswa kumuamini kwani Mungu
kaamua kumleta mtu wake na ni vema kuhakikisha hatupotezi bahati hii.
Mh. Davis Mosha akisalimiana na Mgombea mwenza wa Urais Bi Samia Suluhu. |
Ikumbukwe uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika tarehe 25
Oktoba ambapo wewe mpiga kura unakumbushwa kujitokeza kupiga kura kwa kiongozi
ambaye atakuletea maendeleo na sio mwenye maneno mengi.
Kwa jimbo la Moshi
Davis Elisa Mosha anatosha.
Post a Comment