Mgombea ubunge kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi Mh.
Davis Mosha Leo jioni amefanya ziara ya Ghafla katika Hospitali ya Mawenzi
mjini Moshi kujionea mazingira halisi ya hospitali hiyo hasa zaidi katika wodi
ya Wazazi.
Mh. Davis Mosha akiingia Hospital ya Mawenzi. |
Mh. Davis Mosha alichukua maamuzi hayo kwa kusitisha ratiba
yake ya jioni na kwenda katika hospitali hiyo baada ya kukutana na Mama mmoja
mkazi w kata ya Pasua na kulalamika gharama kubwa wanayotozwa wakina mama
katika kupata huduma ya kujifungua. Alikizungumza kwa uchungu mama huyo ambaye mtoto
wake amelazwa katika wodi hiyo amejikuta akulipa zaidi ya shilingi laki moja
huku akitozwa kiasi cha shilingi elfu Tano kama tozo ya kitanda baada ya siku
tatu za bure za kukaa hospialini hapo.
Mh. Davis Mosha akizungumza na Mzazi ndani ya Wodi ya wazazi. |
Davis Mosha alishangazwa na malalamiko hayo huku akifahamu
huduma kwa wajawazito hutolewa bure katika hospitali hiyo kwa mujibu wa taarifa
ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ambayo inaongozwa na Chadema. Mh Davis
alienda na kujiopnea hali halisi na kuzungumza na wamama wajawazito na ambao
walikua wamekwisha jifungua na kukuta malalamiko hayo ni kweli na kugundua kuwa
wananchi wa Moshi wanadanganywa kwa taarifa ambazo si kweli na wanapopata
matatizo hujikuta wakikabiliana na gharama ambazo zinawalazimu kuzilipa ili
kupata huduma.
Mh. Davis Mosha akiwa na mmoja wa watoto mapacha waliozaliwa leo. |
Mh. Davis Mosha aliwaasa wakina mama hao kuweza kutumia kura
yao kwa usahihi katika kipindi hichi cha uchaguzi ili kumchagua kiongozi ambaye
hatodanganya na atawatekelezea ahadi zao ipasavyo. Pia aliwea kuweka wazi kuwa
huduma nzuri kwa wajawazito ipo katika ilani ya Chama cha mapinduzi na ndio
ilani pekee inayotekelezeka cha muhimu ni kuchagua CCM ili kuweza kutekeleza
mahitaji hayo.
Mh. Davis Mosha akizungumza na wazazi dani ya Wodi ya Wazazi Mawenzi. |
Ikumbukwe Mh. Davis Elisa Mosha ni Mgombea Pekee ambaye
anaweza kuleta mabadiliko ndani ya jimbo la Moshi na itakapofika mwezi oktoba
25 usisite kutoa kura yako ya ndio kwake.
Mh. Davis Mosha akiwa na Mtoto ndani ya Wodi ya Wazazi Mawenzi. |
Post a Comment