0

Waandamaji wakiwa na Mabango nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa

Chama cha mapiduzi wilaya ya Moshi mjini  leo kimefanya maandamano ya amani kuelekea kwa Mwenyekiti wa Ulinzi na usalama wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kupinga vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa wanachama wa ccm wilaya ya Moshi mjini.


Mh. Davis Mosha akiongoza maandamano leo

Katika matukio kadhaa ambayo yameripotiwa kutendeka mara kwa mara katika mikutano ya ccm na misafara ya ccm kushambuliwa kwa mawe na vijana wanaosadikiwa ni wafuasi wa Chadema. Katika mkutano wa Mgombea ubunge kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi jimbo la Moshi mjini Mh. Davis Elisa Mosha Uliofanyika kata ya Rau Mkutano huo ulishambuliwa kwa mawe na vijana hao wanaosadiliwa ni wa chadema na tu na tukio hilo limejeruhi wafuasi wa chama cha mapinduzi na raia na kuharibu mali zao. Pamoja na tukio hilo kuna matukio mengine likiwemo la Mkutano wa Kata ya njoro baada ya kuibuka mwanachama wa Chadema akiwa na panga na kutaka kumshambulia Davis Mosha.

Waandamaji wakiwa eneo la Majengo kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


Katika tukio ambalo limeumiza watu zaidi ni tukio lililotokea Eneo la kiboriloni baada ya msafara wa Mh. Davis Mosha kushambuliwa kwa mawe na kuharibu magari na kujeruhi watu. Mmoja wa Majeruhi ni kijana Nsa Job aliyekua mchezaji wa timu ya Yanga kujeruhiwa kwa jiwe lililopiga koo cha gari na kumjeruhi kichwani na mpaka sasa yupo chumba maalum ICU hajitambui baada ya kufanyiwa Upasuaji wa kichwa.

Mh. Davis Mosha alipokwenda kumtembelea mmoja wa Majeruhi Ndugu Nsa Job



Akipokea maamdamano hayo Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Mh. Novatus Makunga alisema Serikali imesikia malalamiko hayo na serikali yetu ni tiifu inafanyia kazi malalamiko hayo. Pia alitoa Taarifa ya vijana kumi na tano walioripotiwa kufanya vurugu na kujeruhi watu tayari wamekamatwa na wamepandishwa mahakamani. Pia alijibu malalamiko ya wananchi wengi juu ya Mgombea Udiwani wa Kata ya Kiboriloni ndugu Kagoma kuongoza Matukio ya Mashambulizi na Polisi hawamkamati Mh. Makunga amesema suala hilo linafanyiwa kazi na ameagiza Polisi kupeleka ripoti ya mtu huyo mapema ofisini kwake.

Mmoja wa vijana wa ccm waliojeruhiwa na Wafuasi wa Chadema.


Mh. Davis Mosha aliwaasa wakazi wa Moshi na wanachama wa ccm kuwa watulivu katika kipindi hichi cha Uchaguzi na wawe na imani na Jeshi la polisi watahakikisha ulinzi wao katika kipindi cha uchaguzi.

Mke wa Mh. Davis Mosha Bi. Nance Mosha akiwa katika maandamano ya Amani Mjini Moshi leo.




Kaimu mkuu wa mkoa Mh. Novatus Makunga akisikiliza waandamaji nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa 

Mamia ya wanachana na wananchi wa Moshi Mjini wakiwa nje ya ofisi ya mkuu wa Mkoa.

Post a Comment

 
Top