Mh. Magufuli Akimnadi Mgombea ubunge wa Moshi Mjini Mh. Davis Elisa Mosha. |
Mkutano wa Kampezi za Mgombea Urais Kupitia tiketi ya Chama cha
Mapinduzi ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro umeendelea leo kwa kufanyika katika
Jimbo la Moshi mjini. Mkutano huo uliofanyika leo Alaasiri katika Viwanja vya
Mashujaa ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa CCM wa Wilaya, Mkoa na Kitaifa.
Wagombea na viongozi mbalimbali wakiimba wimbo maalumu wa Amani na Umoja. |
Mbali na Mgombea Urais kupitia Tiketi ya CCM ndugu John
Pombe Magufuli alikuwepo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ccm na Mlezi wa Mkoa wa
Kilimanjaro Ndhugu Emanuel Nchimbi. Pia kati ya watu walioongoza Msafara huo ni
Pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Simanjiro Mh. Ole Sendeka.
Akizungumza na Wakazi wa Moshi Mjini Mh. Ole Sendeka
aliwasihi wanachama wa CCM na wapenzi wa CCM kuepukana na Kuwajibu wanachama na
Wafuasi wa Vyama vinavyounda ukawa kwasababu Ukawa wamedhamiria kuchokoza wana
ccm ili kutokee MAchafuko ambayo Nchi za Magharibi zitaona ni CCM ndio wameleta
vurugu.
Mh. John Magufuli akizungumza na Halaiki ya watu mjini Moshi. |
Akizungumza na wakazi wa Moshi Leo Mgombea Urais Mh. John
Pombe Magufuli aliweza kumzungumzia Mh. Davis Mosha ambaye ni Mgombea ubunge
Kupitia Tiketi ya CCM ndani ya Jimbo la Moshi mjini. Magufuli alisema Hana
shaka na Davis Mosha kwa kuwa anaelewa ni Mchapakazi na Mtekelezaji. Amekua
mmoja wa Vijana wa kitanzania wenye mafanikio Makubwa kwa kuwekeza vyema katika
nchi yetu ya Tanzania. Mh. Magufuli alimuahidi Ndugu Mosha kilometa kumi ya
lami ndani ya Jimbo la Moshi mjini iwapo tu wana Moshi watamchagua.
“Davis Aliniambia kuwa Moshi inamaeneo Mengi Muhimu ambayo
Barabara zake sio kiwango cha Lami, Na mimi namuahidi Nitamletea Kilometa kumi
za Barabara ndani ya Moshi Mjini”
Alisema Mh. Magufuli huku Akishangiliwa na Umati mkubwa wa
watu.
Halaiki ya watu katika mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais na Ubunge wa ccm |
Hata hivyo Mh. Davis Mosha aliwaasa wananchi wa Moshi Mjini
wasifanye makosa na kuwaambia huu ni wakati wa maendeleo na Moshi Mjini itajengwa
na watu wa Moshi hivyo wampatie Kura za Urais kwa Dr. John Pombe MAgufuli na
Kura za Ubunge kwa Davis Mosha huku Madiwani wapewe wa Chama cha Mapinduzi ili
kuweza kufanya kazi kwa Pamoja ya Maendeleo ya Moshi Mjini.
Mh. Davis Mosha Mwenye shati la njano wapili kulia akiongoza Madiwani wake katika zoezi la Nguvu na Afya. |
Mh. Davis Mosha akiwa na Wakereketwa wa ccm Moshi Mjini |
Post a Comment