Nia thabiti ya Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM Ndugu Davis
Mosha imeanza Rasmi mapema leo baada ya Mgombea huyo kuchukua Fomu za kuwania
Ubunge ndani ya Jimbo la Moshi Mjini.
Uamuzi huo wa kulitaka
jimbo hilo unathibitisha kauli zake ambazo amezitoa jana katika mkutano wa
waandishi wa habari kuwa ana nia ya dhati ya kulikomboa jimbo la Moshi mjini na
atahakikisha anatumia muda vizuri katika kuanza mchakato wa kukamilisha
taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kukamilika kwa mchakato wa
ndani ya chama wa kumpa ridhaa ya kugombea kupitia chama cha mapinduzi.
Mh. Devis Mosha akiwa na Fomu ya Kugombea ubunge nje ya Ofisi ya Hlmashauri ya manispaa ya Moshi pichani pamoja na mtoto wake Daniella Davis |
Akikabidhiwa fomu ya
Kugombea nafasi ya hiyo ya Ubunge mbele na Msimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
ndani ya Jimbo la Moshi ndugu Shabani Mtarambe ndani ya ofisi ya Halmashauri ya
manispaa ya Moshi. Mgombea huyo aliongozana na Mwenyekiti wa ccm wilaya ya
Moshi mjini Bi. Elizabeth Minde, Katibu wa ccm Wilaya ya Moshi Mjini ndugu Loth
Olemesele, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya ccm Taifa kupitia wilaya ya Moshi Mjini
na Kamanda wa Vijana wilaya ndugu Agrey Marealle, Mwenyekiti wa UVCCM Moshi
Mjini Ndugu Abdallah Thabit pamoja na Mke wake Mrs Davis Mosha na watoto wake
Edger Devis Mosha na Daniella Devis Mosha.
Viongozi wa ccm wakimsindikiza Davis Mosha kuchukua fomu katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi |
Akizungumza baada ya
kukabidhiwa Fomu hiyo Ndugu Davis Mosha alisema hakuona haja ya kusubiri zaidi
ya kutimiza jukumu ambalo wananchi wa Moshi Mjini wanatarajia kumtuma hivyo
basi akaona ni vyema kuwahi tiketi yake mapema ambayo itamuwezesha kugombania
nafasi hiyo na tiketi hiyo ni Fomu ya Kugombea nafasi ya Ubunge inayotolewa na Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuahidi kuijaza kwa kufuata maelekezo aliyopata
kutoka katika tume hiyo ili kuhakikisha anaingia katika kinyang’anyiro cha
ukombozi wa jimbo hilo.
Hata hivyo Msimamizi
wa Uchaguzi ndani ya Jimbo la Moshi mjini alitoa Pongezi kwa mgombea huyo kwa
kuongoza kwa kuwa wakwanza kuchukua fomu
kati ya wagombea wa vyama mbalimbali walioomba nafasi hiyo. Lakini pia alichukua
nafasi hiyo kuwasihi wagombea uunge kuhakikisha wanajaza fomu hizo kwa
uangalifu na umakini mkubwa kulngana na maelekezo yaliyotolewa na tume hiyo.
Post a Comment