Mgombea Ubunge kupitia Tiketi ya Chama cha mapinduzi ndani
ya jimbo la Moshi Mjini Mh. Davis Elisa Mosha
Amepokea barua ya kutambuliwa rasmi kama mgombea ubunge kupitia ccm,
Barua hiyo aliyopokea mapema leo katika ofisi chama cha mapinduzi mkoa wa
Kilimanjaro Ndugu Davis Mosha alishukuru sana wanachama wa chama cha mapinduzi
kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kuwakilisha katika nafasi hiyo yenye dhamana
kubwa katika uongozi.
Baada ya kupokea barua hiyo Mh. Davis Mosha alikutana na
waandishi wa habari katika Hoteli ya Nyumbani Hotel na kuzungumza nao juu ya
Adhma yake ya kulikomboa Jimbo la Moshi Mjini. Aliweza kuzungumzia mustakabali
wa jimbo la Moshi huku akitoa wito kwa wakazi wa Moshi mjini kujitokeza katika
mikutano yake na kusikiliza sera na mikakati yake ya maendeleo ndani ya jimbo
la Moshi ili kuweza kumpima na kufanya maamuzi sahihi.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari Mgombea ubunge huyo
aliweka wazi juu ya tetesi zilizokua zimezagaa kuhusu jina lake kukatwa na
kamati kuu ya ccm. Davis alisema Chama cha mapinduzi kina imani nae na
kimetumia demokrasia na kuthamini maamuzi ya wanachama wake wa jimbo la Moshi
lakini pia wanaamini Jimbo la Moshi linahitaji mtu sahihi mwenye weledi wa
uongozi na mwenye uwezo wa kuleta maendeleo Jimboni
|
Mh. Davis mosha akizungumza na makatibu wa ccm wa kata ndani ya ukumbi wa ccm mkoa mapema leo baada ya kutambulishwa rasmi kama mgombea ubunge ndani ya jimbo la Moshi mjini. |
|
Mamia ya Makatibu wa ccm wilaya ya Moshi mjini wakimsikiliza Mh. Davis Mosha a.k.a Jembe ndani ya ccm Mkoa leo. |
|
Mh. Davis mosha akionesha barua Rasmi ya kuchaguliwa kugombea ubunge
ndani ya Jimbo la Moshi Mjini mbele ya waandishi wa habari. |
|
Mwandishi wa Habari akiuliza swali kwa Mh Davis Mosha |
|
Mh. Davis mosha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari |
|
Wandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mh Davis Mosha |
Post a Comment