0




Chama cha Mapindizi jana kiliendesha mchakato wa kuwapigia kura wanachama waliojitokeza kuwania nafasi za ubunge na Udiwani katika Wilaya mbalimbali Nchini. Katika Mji wa Moshi wagombea Takribani kumi na mbili waliomba ridhaa ya kuchaguliwa huku Miongoni mwao akiwemo Mfanyabiashara mkazi wa Kiboriloni moshi mjini Ndugu Davis Mosha. Mpaka kufika saa kumi na nusu zoezi la upigaji kura lilikua limekwisha kwa amani na taratibu za majumuisho ya kura katika vituo zilianza. 

Ilipofika mnamo saa kumi na mbili matokeo yalianza kujulikana kupitia mawakala wa wagombea walio katika vituo na kupitia matokeo hayo mpaka kufika saa moja usiku Davis mosha alikua naongoza ka kura 5271 huku mgombea aliyemfuata akiwa ana kura 700. Hayo yakiwa ni majumuisho ya vituo 50 kati ya vituo 61 vilivyopiga kura. Hivyo kutokana na matokeo hayo Tayari Dalili ilionesha Ndugu Davis Mosha kushinda kwa kishindo katika mchakato huo. Hivyo ndipo wanachama wa CCM na wananchi wa Moshi mjini wakashindwa kuzuia hisia zao na kuanza kufurahia kwa ushidi huo huku wakiwa na tumaini jipya kutoka kwa Davis Mosha juu ya Jimbo la Moshi.

Ikumbukwe ni miaka ishirini sasa Jimbo la moshi linaongozwa na Upinzani sasa ni wakati wa Mabadiliko yenye dhamira ya kweli.


Mh. Davis Mosha akitete jambo na Hendrew Mpiganaji ngumi za kulipwa wa zamani nje ya ofisi za CCM Wilaya ya Moshi mjini



Davis Mosha akiwa na wananchi wa wilaya ya Moshi Mjini
Davis Mosha akiwa na Kamanda wa Vijana Wilaya ya Moshi Mjini na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM ndugu Agrey Marealle, Nje ya Ofisi ya CCM Wilaya ya Moshi

Mh. Davis Mosha akiwa na wanachama wa ccm baada ya majumuisho ya matokeo ya awali kutoka kwa mawakala wa vituo kuonesha ameshinda kwa kishindo.



Waendesha pikipiki wakifurahia ushindi wa Mh. Davis Mosha
Mh. Davis mosha akizungumza na wanachama waliokuja nje ya nyumba yake kumpongeza.


Mh. Davis mosha hakusita kuonesha furaha yake kwa wapiga kura wake

Marafiki na wafanyaiashara Hawakua nyuma kuhakikisha Jimbo linakombolewa.


Furaha inapozidi unashindwa kuzungumza na kubaki na zawadi ya Tabasamu.
"Nawashukuru sana tuendelee na umoja wetuu"
Mh. Davis Mosha akiingia katika Tafrija ya Fmilia ya Mama Anna Mkapa aliyoalikwa kwa heshima. Pembeni ni William Malecela (Le Mutuz)
Mh. Rais Mstaafu ndugu Benjamin Wiliam Mkapa akimpa mkono wa Pongezi Mh. Davis Mosha
"Hongera sana"
Mama Anna Mkapa akimpongeza Mh. Devis Mosha

Post a Comment

 
Top