0
Mgombea nafasi ya Ubunge katika kura za Maoni kupitia chama cha mapinduzi Mh. Davis Mosha Amesimamisha mji wa Moshi kwa Saa mbili mfululizo baada ya Matokeo ya kura za Maoni kutangazwa. Matokeo yalipotangazwa nje ya ofisi za ccm wilaya ya Moshi Mjini. Baada ya kuongoza kwa kura 5271 sawa na asilimia 75% huku mpinzani wake mkubwa ndugu Boisafi akijikongoja kwa kuambulia kura 761 sawa na asilimia 11% 

Wanachama wa ccm walishindwa kuzuia furaha yao na kujikuta wakifanya tukio ambalo ndugu Mosha hakulitegemea kwa kutembea nae zaidi ya kilometa 60 kuzunguka katika kata za Manispaa ya Moshi. Hii ikiwa ni ishara kuwa wanachama wameridhishwa na matokeo hayo pamoja na kuridhishwa na mgombea waliyemuhitaji. Kutokana na Matokeo hayo ambayo Mh. Davis mosha ameongoza katika vituo zaidi ya 50 vya kupigia kura kunampelekea kutangazwa mshindi wa kura za maoni na jina lake kwenda katika Kamati kuu ili kujadiliwa kabla ya kukabidhiwa Dhamana ya kupeperusha bendera ya ccm ndani ya jimbo la Moshi Mjini.



Mh. Davis Mosha akiingia katika ofisi ya ccm wilaya ya Moshi Mjni


Mh. Davis Mosha akikumbatiwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ccm Bi. elizabeth Minde



Kamanda wa vijana ccm wilaya ya Moshi Mjini Mh. Agrey Marealle akiingia katika ofisi za ccm Wilaya ya Moshi mjini


Wanachama wa ccm wakiwa nje ya ofisi ya cm wilaya ya Moshi mjini
Wagombea wakiwa katika kikao cha majumuisho ya matokeo

Wanachama na wanahabari wakisubiri matokeo kwa hamu

Matokeo ya kura za maoni yakisomwa nje ya ofisi ya ccm



Wanachama wa ccm wakishangilia baada ya matokeo kutangazwa


Mmoja wa wagombea ndugu Priscus tarimo akimpongeza Davis Mosha baada ya kutangazwa kwa matokeo.


Haya ndiyo matokeo rasmi ya kura za maoni







Wanachama wakishangilia huku wakitembea na Mh. Davis Mosha

Mh. Davis Mosha akiwa katika Maandamano na wanachama wa ccm

Furaha inapozidi hata chini nitalala

Kilometa zaidi ya sitini bila kuchoka

Kila alipopita hakuchoka kusimama na kushukuru wanachama waliomchagua


Mh. Davis Mosha akizungumza na wanachama wa kata ya njoro
Furaha imepitilizaa

Mh. Davis Mosha akiongea na wanachama wa ccm baada ya kutembea zaidi ya kilometa 60 na kumalizia kata ya kiboriloni.

Post a Comment

 
Top