Mshindi wa Kura za Maoni kwa kiti cha ubunge kupitia chama cha mapinduzi, ndani ya jimbo la Moshi Mjini na Mfanyabiashara nchini Tanzania Ndugu Davis Elisa Mosha ameonja adha ya Mtandao siku ya leo baada ya mtu asiyefahamika kutengeneza ukurasa wa Facebook wenye jina lake na kuanza kutuma taarifa za uongo.
Mh. Davis mosha akizungumza na Mwenyekiti Mstaafu wa ccm Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Peter Davie |
Tukio hilo limeanza asubuhi ya leo baada ya watu mbalimbali kuanza kumpigia simu na kumuuliza juu ya taarifa zake zilizoko katika mtandao. Baada ya kupokea Taarifa hizo aliweza kuhakikisha na kukuta ni kweli na picha zilizopo katika ukurasa huo ni za kwake huku maelezo yaliyowekwa katika picha hizo yakiwa si sawa na picha. Hata hivyo Davis Mosha aliweza kwenda mbali zaidi na kuripoti tukio hilo katika vyombo husika vya uhalifu wa mtandao huku akiitaarifu mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na mamlaka hiyo kumuahidi kuhakikisha wanampata muhusika huyo.
Huu ndio ukurasa Feki wa facebook wenye jina la Davis Mosha ambao unasambazwa katika Mitandao |
Davis Mosha aliweza kuzungumzia kwa undani zaidi kuhusu hilo na kusema kuwa hili suala limetokea baada ya kuonesha nia ya kugombea ubunge ndani ya jimbo la Moshi na kuona hizo ni sababu za kisiasa ambazo zina lengo la kumkatisha tamaa ya kuwatumikia wananchi wa Moshi mjini ambao ameona ni wakati sahihi kurudi nyumbani na kuujenga mji wa Moshi pamoja na ndugu zake wa Moshi. Hata hivyo amewatahadharisha wale wote wenye nia ya kumkatisha tamaa kuwa hatoweza kukata tamaa na katika maisha yake ya kila siku hajawahi kukata tamaa, Na ana nia ya dhati ya kusaidia ndugu zake wa Moshi Mjini.
Mh. Davis Mosha akizungumza na wananchi pamoja na wanachama waliokuja nyumbani kwake kumpongeza baada ya ushindi wa kura za maoni. |
Hata hivyo tuliweza kuongea na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ndugu Inocent Mungi kuhusu tukio hilo aliweza kuwatadharisha watanzania juu ya matumizi mazuri ya mtandao hasa kuhusu taarifa binafsi za mtu. Katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi ni vyema kuwa makini na upokeaji na utumaji wa taarifa ambazo si sahihi na kama huna uhakika nazo zinaweza kukuingiza katika uhalifu wa mtandao na kushtakiwa kisheria. Na suala la mtu ambaye ametenda kosa hilo kwa kutengeneza ukurasa wa jina la Davis Mosha atapatikana na sheria itachukua mkondo wake.
Post a Comment