0
Ushirika Veteran ni moja ya timu za maveteran Nchini Tanzania zenye ushindani mkubwa katika Mchezo wa Mpira wa Miguu. Timu hiyo ya Maveteran wa mpira wa Miguu iliyounganisha wachezaji na wapenzi wa mchezo wa ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro. Katika kuadhimisha sikukuu ya wakulima Timu ya Ushirika Veteran wameandaa Bonanza la Mpira wa Miguu ndani katika uwanja wa nyumbani uliopo ndani ya Chuo cha Ushirika Moshi (Mucco).
Wachezaji wa Ushirika veteran wakifurahi baada ya kuichapa timu ya bagamoya goli 3 kwa 2





 Wachezaji wa Bagamoyo Veterani wajijadili jambo baada ya kushindwa kufurukuta dhidi ya Ushirika veteran

Bonanza hilo lililoanza mapema asubuhi ya leo likiwa linashirikisha timu mbalimbali za Maveterani kutoka sehemu mbalimbali Tanzania. Timu zilizoshiriki katika Bonanza hilo ni timu ya Bagamoyo, Arusha wazee, Mwangaza na Ushirika Veteran. Timu zote hizi zitashindana katika mchezo wa mpira wa Miguu, Kukimbiza kukuna kukimbia kwa Magunia. Akizungumza na Mwandishi wetu Mratibu wa Bonanza hilo ndugu Kusi Kiata alisema Nia ya kuandaa Bonanza hili ni kufanya mazoezi ili kuimarisha afya lakini pia kujenga mahusiano kati ya timu za Maveterani.

Maveteran wakikimbiza kuku katika mchezo wa kukibiza kuku.

Bagamoyo Vetran wakiwa wamembeba mchezaji wao baada ya kuibuka mshindi wa kukimbiza kuku.

 Kusi alitoa wito kwa maveterani kwa wadau wa soka kujitokeza kuunga mkono michezo huku Akitoa shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Delina Group kwa kuwezesha Bonanza hilo kufanikiwa japokua walimpa taarifa ndani ya kipindi kifupi lakini aliunga mkono moja kwa moja hiyo inaonesha ni kiasi gani anathamini michezo.Bonanza hilo liliisha saa kumi na mbili kamili kwa Ushirika Veteran kuibuka na Ushindi kwa mechi ya fainali iliyoikutanisha Ushirika Veteran na Mwangaza na Ushiika Veteran kuiadhibu Mwangaza Goli 5 kwa 2 na kupelekea Ushirika Veteran kuibuka kidedea wa Bonanza hilo.

Timu ya Wazee Veteran ya Arusha ikimenyana na Timu ya Mwangaza Veteran ya Arusha katika uwanja wa Ushirika
Mashabiki wakifuatilia Bonanza hilo

Post a Comment

 
Top