0
Mgombea Ubunge kupitia Tiketi ya Chama cha mapinduzi ndani ya Jimbo la Moshi Mjini Mh. Davis E. Mosha amehudhuria Misa ya kumuaga Mwanasiasa Mashuhuri Muasisi wa Tanu na Chama cha Mapinduzi Marehemu Peter Kisumo.  Marehemu Peter Kisumo aliyefariki Tarehe 03/08/2015  Katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Mzee Peter Kisumo uliwasili nyumbani kwake Shant Town Moshi Mjini jioni ya tarehe 11/08/2015 na kisha kuandaliwa Misa maalumu ya kumuaga kwa wakazi wa Moshi. Misa hiyo ilifanyika katika Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Moshi Mjini.

Mh. Davis Mosha akiwasili Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Moshi Mjini.




Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanasiasa mbalimbali walizungumzia Mchango wa Mzee Peter Kisumo katika siasa za Tanzania na harakati za kutafuta uhuru wa Tanzania.  Mwenyekiti Mstaafu wa ccm mkoa Kilimanjaro Ndugu Peter Davie alisema Anamkumbuka Mzee Peter Kisumo kama mwanasiasa mahiri na mwenye weledi wa uongozi na pindi panapotokea utofauti katika utendaji hakusita kuzungumza na kuonya.

Hata hivyo misa hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali huku kivutio kikubwa ikiwa ni mgombea ubunge kupitia tiketi ya ccm ndugu Davis Mosha kwani alipoingia katika eneo la kanisa hilo wananchi na wanasiasa na viongozi mbalimbali hawakuweza kuficha furaha zao na kujikuta kila mmoja akimpongeza kwa nia yake ya kutaka kukomboa jimbo la Moshi mjini. Kitendo ambacho kilisababisha baadhi yao kushindwa kuficha hisia zao na kusema wamechoshwa na ahadi zisizotekelezeka walizokua wakipewa takribani miaka ishirini sasa na vyama vya upinzani vilivyoongoza jimbo hili kwa miaka yote hiyo.


Mh. Davis Mosha akisalimiana na Mfanyabiashara Maarufu kama Shana boy nje ya kanisa hilo

Mzee Peter kisumo anatarajiwa kuzikwa Tarehe 13/08/2015 nyumbani kwake Usangi ambapo msiba huo utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.



Mh. Davis Mosha akisalimiana na viongozi wa ccm Wilaya ya Moshi Mjini

Mh. davis Mosha akiwa katika misa ya kumuaga Mzee Peter Kisumo

Mh. Davis Mosha akiwa Tayari Kupita kuuaga Mwili wa Marehem Mzee Peter Kisumo
Mh. Davis Mosha akitoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu

Mh Davis Mosha akiwa kanisani katika Misa ya Kumuaga Mzee Peter Kisumo
Mh. Davis Mosha akiwa na Mwenyekiti Mstaafu wa ccm Mkoa wa Kilimanjaro Mzee Peter Davie

Mh. Davis Mosha akisalimiana na Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Moshi mjini Bi. Elizabeth Minde

Mh. Davis Mosha akisalimiana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania usharika wa Moshi mjini Baba Askofu Shoo.

Baba Askofu Shoo akiwa na Mh. Davis Mosha katika kanisa la Lutheran usharika wa Moshi mjini.

Wananchi wa Moshi mjini wakiteta jambo na Mh. Davis Mosha nje ya kanisa baaa ya Misa ya Kumuaga mzee Peter Kisumo

Post a Comment

 
Top