|
Mgombea Ubunge Moshi Mjini Davis Elisa Mosha |
Mgombea ubunge Kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi ndani
ya Jimbo la Moshi Mjini. Mh Davis Elisa Mosha amezidi kuonesha ushupavu wake
katika uongozi na jinsi alivyo na hari ya kutatua changamoto zinazowakabili
wakazi wa Moshi Mjini. Hilo limejionesha tokea kipenga cha kampeni za uchaguzi
kilipopulizwa na kuanza kutaka kujua kero mbalimbali za wananchi kwa kutembelea
maeneo husika.
Davis akitumia aina ambayo inawachanganya wapinzani wake na
bila kujua atakuwa wapi amekua akitokeza katika maeneo mbalimbali bila taarifa
na kuzungumza na wakazi wa eneo hilo huku akitazama changamoto zao na kuweka
mikakati ya kuzifanyia kazi. Akiwa katika Soko la Mbuyuni Mapema wiki hii Davis
alizungumza na wakina mama wafanyabishara wa soko hilo na klupokea changamoto
mbalimbali zinazowakabili na kuwaahidi kuzifanyia kazi mapema.
“Natamani ningeanza kazi Sasa hivi kuondoa hizi kero na
kinachonishangaza kwanini mnaishi katika soko ambalo mnalipia mapato lakini
hakuna Maji safi na salama” Davis aliwaambia wafanyabiashara wa Soko la
Manyema.
Ikiwa Kampeni zinazidi kushika kasi ndani ya jimbo hilo
Davis Elisa Mosha amefanya mikutano kadhaa na kuweza kuzungumza na wananchi juu
ya maendeleo ya Jombo la Moshi. “Huyu
kijana ni kiongozi kweli na ana nia ya dhati si wakati wa kupoteza watu kama
hawa katika mji wetu wa Moshi ni wakati wa kumchagua na kushirikiana nae”
Alisema Christina Minja Mfanyabiashara wa chakula eneo la Shabaha Moshi.
Tazama Picha zaidi......,
|
Mh. Davis Mosha akiwa na Wazee wa Baraza la wazee ccm |
|
Mh. Davis Mosha akiagana na wazee wa ccm baada ya picha ya pamoja. |
|
|
|
Wananchi na wafanyabiashara ndogondogo wa eneo la Shabaha Moshi mjini wakifurahi pamoja na Mh. Davis Mosha |
|
Mh. Davis Mosha akizindua Shina la wakereketwa wa Soweto MASKANI YA KIKWETE |
|
Mh. Davis Mosha akizungumza na wakazi wa Kata ya Soweto. |
|
|
|
Mh. Davis Mosha akiwanadi wagombea udiwani wa kata ya Soweto, Karanga na Shirimatunda |
|
|
|
Wananchi wa Moshi mjini wakiwa katika Moja ya Mikutano ya Kampeni za Mh. Davis Mosha |
|
|
|
Mh. Davis Mosha akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Manyema. |
|
|
|
Mh. Davis Mosha akisalimiana na Mfanyabiashara ndogondogo wa soko la Mbuyuni baada ya kuzungumza nao alipowakuta wakipata chakula mchana. | | |
|
|
|
Mh Davis Mosha akisalimia alipopita katika kampeni za Mgombea Udiwani wa Korongoni. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mh. Davis Mosha akiondoka katika baada ya Mkutano wa Kampeni wa Soweto |
Post a Comment