0
Mh. Davis Mosha akiwa na Mjumbe wa kamati kuu ya Ccm Taifa kutoka Wilaya ya Moshi Mjini Mh. Agrey Marealle wakila kiapo cha utii na uaminifu Pamoja na viongozi na mabalozi wa ccm wa wilaya ya Moshi mjini mapema leo.



Leo katika mji wa Moshi tokea mnamo wa saa tano za Asubuhi kulionekana Pilika pilika za watu wakipita katikati ya Mji huo wakiwa wamevalia sare za Chama cha Mapinduzi. Mji wa Moshi ukifahamika kati ya Miji yenye ngome ya pinzani kati ya Miji ya Tanzania. Ni nadra sana kwa mwaka mmoja nyuma kukutana na Mwanachama wa ccm kavaa nguo ya ccm kutokana na upinzani uliopo ndani ya Jimbo la Moshi.

Wanachama wa ccm wakionekana katikati ya Mji wa Moshi leo




Hali imekua tofauti tokea Mgombea Ubunge wa Moshi Mjini kupitia Tiketi ya CCM ndugu Davis Elisa Mosha atangazwe kama Mgombea ubunge wa Jimbo hilo kwa Tiketi ya CCM. Mh. Davis Elisa Mosha ameweza kuhakikisha anakijenga chama katika wilaya hiyo ya Moshi mjini na kuwaunganisha pamoja. Katika hilo akafanikiwa kuweza kurudisha mapenzi ya chama kwa wanachama wake.

Viongozi wa ccm zaidi ya elfu tatu wakimsikiliza Mh. Davis Mosha hayupo pichani.


Katika Viwanja vya ccm Mkoa kulikua na Shamrashamra huku vijana, Wazee na wakina Mama wakiwa na sare za ccm wakiingia ndani ya Viwanja vya ofisi hiyo. Hali hii iliashiria tukio ambalo ni muhimu na nadra sana katika Wilaya ya Moshi mjini. Mgombea ubunge wa Moshi Mjini Ndugu Davis Elisa Mosha aliamua kutimiza Moja ya ahadi zake katika chama alizoahidi iwapo atachaguliwa kuwa Mgombea wa ccm basi atafanya kazi ya kukijenga chama na kujenga umoja madhubuti wa chama. KAtika kutekeleza hilo Davis Mosha amewakutanisha Mabalozi wa Nyumba kumi, Makatibu Kata, Makatibu wa Matawi na Mashina wa kata 21 za Manispaa ya Moshi. 

Mh. Davis Mosha akizungumza na maelfu ya viongozi wa ccm mapema leo.


Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, Wilaya na Mkoa. Viongozi waliokuwemo kitaifa ni Pamoja na aliyekua Waziri wa maendeleo ya jamii wanawake na watoto Bi. Sofia Simba. Mosha aliweza kuwaeleza wanachama wa ccm huu ni wakati wa kukijenga chama huku akikumbushia wakati alipokua chipukizi wa ccm chama kilikua na nguvu ndani ya Moshi na kilikua ni muhimili mkubwa sana katika wilaya ya Moshi. Aliwaasa wanachama na viongozi hao kufanya sala kila mara kukiombea chama na pia kulinda kura za ccm ambazo wanazo mkononi akimaanisha kitambulisho cha kupigia kura. Pia aliwaasa kuhakikisha wanahamasishana kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura na kuilinda amani yetu ya Moshi ambayo imeanza kuhubiriwa vibaya na wapinzani huku wakitaka kuiharibu wakitumia mwamvuli wa chama cha mapinduzi. 

Kwa upande wake aliyekua Waziri wa Maendeleo ya jamii watoto na wanawake Bi Sofia Simba alisema hakutegemea anachokiona mbele ya macho yake na hajapata kuona kiongozi ambaye anaweza kukijenga chama kwa kuwaunganisha wanachama pamoja huku akimshushi Mh. Davis Elisa Mosha sifa za kutimiza ahadi yake kwa chama kabla ya kuwa Mbunge na kumalizia akisema. 
"Davis Mwanangu Umevunja Rekodi"

Mh. Davis Mosha akiwa na Madiwani wake akifurahia jambo na Balozi wa ccm leo.


Mabalozi na viongozi wa ccm wakicheza pamoja na Mh. Davis Elisa Mosha alipokua akiimba na kucheza leo.












Mh. Sofia Simba akimkabidhi Mh. Davis Mosha kwa viongozi wa ccm Moshi Mjini

Post a Comment

 
Top