0
Mh. Davis Mosha akiwa anaingia kwenye Mkutano kata ya Miembeni



Pilika pilika ya kampeni za Ubunge ndani ya jimbo la Moshi mjini zinazidi kushika kasi huku Mgombea Ubunge wa ccm Ndugu Davis Mosha leo akifanya mkutano Mkubwa wa hadhara katika kata ya Miembeni. Katika mkutano huo Mh. Davis Mosha aliweza kusikiliza changamoto mbalimbali za wakazi wa eneo hilo na kuahidi kuzitatua huku akiwasisitiza Kumchagua Diwani wa eneo hilo Maarufu kakma Babu Jumaa.


Mamia ya wakazi wa kata ya Miembeni Waimsikiliza Mh. Davis Mosha
 Hata hivyo katika hali isiyotarajiwa umoja wa kabila la wasambaa wanaoishi Moshi mjini waliweza kutoa malalamiko yao kwa Mh. Davis Mosha juu ya Mgombea Udiwani kwa tiketi ya Chadema Mh. Jomba Koi kwa kuwatukana wasambaa wa Njoro. Kutokana na Mashtaka hayo Davis Mosha aliomba wasambaa hao kuhakikisha wanamnyima kura yeyye na Mbunge wake kama Adhabu ya Ubaguzi waliouonesha na kuasa jamii kuwakataa viongozi ambao wanahubiri ubaguzi wa makazi, kabila rangi au Dini.



Mh. Davis Mosha akizungumza na wakazi wa Kata ya Miembeni

Pia Davis Mosha hakusita kuainisha vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa kuwa mgombea ikiwa ni Kuwezesha vikundi vya kina mama, Vijana na wazee. Pia kuwawezesha Vijana waliojiajiri kupitia pikipiki maarufu kama bodaboda kwa kuwawezesha katika sacos zao kuweza kuwakopesha pikipiki na watatumia kama mradi wa kujikopesha. Pia Davis hakuwasahau wakina mama wajasiriamali ambao wanavikundi vya kukopeshana huku akiwaambia juu ya msaada kutoka kwa wafanyabiashara wenzake wa zaidi ya milioni mia tano ambazo atazitoa katika vikundi vya wajasiriamali.


 
Mariam Ditopile akinadi sera za ccm katika mkutano wa Mgombea ubunge Moshi mjini Mh. Davis Mosha.



Mamia ya wakazi wa Kata ya Miembeni walionesha moyo wa furaha na kulipuka kwa shangwe huku wakiwa na imani juu ya Davis Mosha.


Mamia ya wananchi wa Miembeni wakifurahi baada ya Mh. Davis Mosha kumaliza kuzungumza nao

Post a Comment

 
Top