Mh Davis Mosha akiwa na Mwenyekiti wa KDFAA Ndugu Msasu. |
Mgombea Ubunge wa Moshi Mjini kupitia Tiketi ya ccm Mh.
Davis Mosha Amekutana na wasanii wa Filamu, Maigizo ya Jukwaani, Sarakasi na
Muziki wa Mjini moshi. Wasanii hao wakiongozwa na Chama cha Wigizaji na wacheza
filam Kilimanjaro (KDFAA)
Wasanii wakimsikiliza Mh. Davis Mosha wakati akizungumza nao Leo jioni. |
Wasanii hao walioomba Mkutano na Mh. Davis Mosha leo katika
ukumbi wa ccm Mkoa walipata fursa ya kuzungumza Changamoto zinazowakabili na
Malengo yao kama wasanii wa Moshi na Mkoa Kilimanjaro. Wakiongea kwa nyakati
tofauti katika ukumbu huo mmoja wa Wasanii wa Muziki Ndugu Samwel Stephen aliweza
kumuomba Mh. Davis Mosha awasaidie kupata studio ya kisasa na kuwapa wigo mpana
wa kazi zao za muziki kuweza kupigwa katika Radio.
Mh. Davis Mosha akijibu hilo aliwahakikishia Kujenga Studio
ya Kisasa itakayoanza kufanya kazi mapema Mwezi ujao chini ya Kampuni yake ya
African Swahili Media sambamba na Kufungua kituo cha Redio na Tv.
Wasanii wa Filamu waliomba kuweza kusaidiwa kurekodi
Tamthilia ambayo itaweza kurushwa katika Tv na waweze kujitangaza na kujiajiri
kupitia sanaa hiyo lakini pia hawakusita kutoa kilio chao juu ya Wizi wa kazi
zao unaofanywa na wasambazaji pamoja na Wasambazaji kutoka Dar es Salaam
kuwanyonya na kusababisha kazi zao za Film kubaki nyumbani badala ya kwenda
Sokoni. Pia waliweza kutoa malalamiko yao juu ya uongozi uliokuwepo madarakani
katika ngazi ya ubunge na Udiwani kuwaahidi maramara ahadi ambazo
hazitekelezeki.
Mh Davis Mosha akifafanua Jambo katika Mkutano na Wasanii Leo |
Bwana Mosha aliweza kuwahakikishia Soko la uhakika la filam
zao na pia ulinzi wa kazi zao kupitia vyombo husika vinavyoshughulikia masuala
ya haki miliki na pia kuweza kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao. Na pia
aligusia suala la wasanii wa Ngoma za asili juu ya kuhakikisha anaweka kituo
cha sanaa na utalii ili kuweza kuwakutanisha wageni wanaokuja kupanda mlima na
kufanya ni kituo cha kubuudika kupitia ngoma za asili na sehemu ya kujifunzi
aTamaduni za Makabila mbalimbali ya Tanzania. LAkini pia aliwaasa wasanii kutumia
sanaa yao kutoa elimu ya uchaguzi juu ya wananchi kutumia haki yao ya msingi
katika kuchagua na wasifanye makosa watumie Mitaji yao ya Vitambulisho vya
kupigia kura kuhakikisha wanachagua Kiongozi atakayeenda kufanya kazi na si
mwanasiasa.
Mwenyekiti wa KDFAA akitoa shukrani zake kw Mh. Davis Mosha kwa Kukubali kuja kuwasikiliza. |
Post a Comment