0
Mh, Davis Mosha akiwahutubia mamia ya waBondeniazi wa kata ya kata ya Bondeni.





Ikiwa zimesalia Takribani siku ishirini na tisa kuweza kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (ccm) Jimbo la Moshi Mjini Ndugu Davis Elisa Mosha amezidi kumtesa Mpinzani wake kutoka Kambi Pinzani ya Ukawa anayesimama kwa Tiketi ya Chadema Ndugu. Jafary Michael. Hayo yamedhihirika leo katika Mkutano wa Hadhara wa Mh. Davis Mosha katika viwanja vya Manyema vilivyopo kata ya Bondeni. 


Meneja Kampeni wa Mh. Davis Mosha h. Mwita akizungumza na wakazi wa Kata ya Bondeni.
Mkutano huo uliofurika mamia ya wakazi wa katahiyo huku wakionesha furaha ya waziwazi, Wakazi wa Kata hiyo wamesema hawawezi kufanya makosa tena katika kusimamisha Mbunge wa Jimbo la Moshi na watachagua Kingozi sahihi ambaye ni Davis Mosha. 

Wakazi wa kata ya Bondeni wakimsikiliza Mh. Davis Mosha akinadi Sera zake za maendeleo ya Moshi Mjini.
Akizungumza kwa Furaha huku akiwa na Picha ya Mh. Davis Mosha Bi. Veronica  Deus alisema kama ni kiongozi basi Mungu kawaletea Davis Mosha na atampigia kura na atahakikisha analinda kitambulisho chake cha kupiga kura ili aweze kukitumia kumpeleka Davis Mosha Bungeni ili alete Maendeleo. “Unajua huyu kijana Katosheka, Tayari ana fedha zake na Desturi yetu hatuwezi chagua Fukara asiye na fedha, Ndio maana tulimchagua Ndesamburo sababu ana Pesa, Sasa leo unaweza kumfananishaje Jafary na Davis Mosha, Hii ni sawa na Kifo na Usingizi” Alisema Bi Veronica deus.

Mh. Davis Mosha akizungumza na Wakazi wa Kata ya Bondeni
Pamoja na yote Mh. Davis Mosha alisema huu ni wakati wa kufanya vitendo na si maneno ya siasa, Yeye si mwanasiasa ila ni mtendaji na amekuja kushirikiana na wana Moshii kuijenga Moshi tunayoitegemea. “Huu si wakati wa Kulala ni wakati wa Kufanya kweli, Tujumuike Pamoja kufanya kweli kuiondoa chadema tumewapa nafasi muda mrefu na wametumia Halmashauri ya Moshi Mjini kujinufaisha wao. Sasa ni zamuya Wananch I kula matunda ya kodi zao na hakuna mwingine mwenye uwezo huo. Nitumeni mimi” Alisema Mh. Davis Mosha huku akishangiliwa na ummati mkubwa wa watu.

Mke wa Mh. Davis Mosha Madame Nance akisalimu wakazi wa Kata ya Bondeni.







Mh. Davis Mosha akiwaaga  wakazi wa Kata ya Bondeni baada ya kumalizika kwa mkutano.

Post a Comment

 
Top