Hali ambayo haikutarajiwa na
wengi katika Jimbo la Moshi Mjini, Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi ameanza utekelezaji wa ahadi zake katika Jimbo hilo. Baada ya wiki
chache kuzungumza na wanamuziki na wasanii kuhusu kazi zao na wasanii hao
kuomba kupata kituo cha Redio cha kisasa na Studio ya kisasa ambavyo vitaweza
kufanya kazi zao kwa ubora zaidi na pia kufika mbali.
|
Mh. Davis Elisa Mosha |
Katika kutekeleza hilo Mh. Davis Mosha amekwishaanza ujenzi
wa Studio ya Kisasa ya Kituo cha Redio chini ya Kampuni yake ya Africa Swahili
Media na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mapema na vifaa vya Studio huyo
vinatarajiwa kuwasili muda wowote kutoka Dar es Salaam baada ya kuwasili
Bandarini vikitokea Nchini Italy. Mh. Davis Mosha aliwaahidi wasanii hao
kufungua kituo cha Redio kitakachoweza kusikika Tanzania Nzima na Duniani kote
kwa njia ya Satelite. Pia aliwahakikishia kufungua na kituo cha televisheni. Kituo
hicho cha Redio na Studio ya kisasa kianatarajiwa kufunguliwa katika jengo la
Kilimanjaro Commercial Complex Maarufu kama jingo jipya la NSSF lililopo Moshi
Mjini.
|
Hati ya Kontena la Vifaa vya Studio lililotoka Italy Baada ya kuingia Bandari ya jiji la Dar es Salaam. |
Mbali na utekelezaji huo wa Kero ya Wasanii, Mh. Davis Elisa
Mosha wiki iliyopita aliweza kufanya Ziara ya kimya kimya katika Soko la
Mitumba la King George Memorial na kutazama Changamoto za Soko hilo lakini pia
alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Soko hilo na wafanyabiashara wa Soko
hilo. Kwa pamoja walieleza MAzingira magumu wanayofanyia Biashara huku ikiwa
Miundombinu mibovu ikiwemo vyoo na Soko halina Paa inapelelea iwapo mvua
itanyesha basi kunakua hakuna biashara kabisa maana Bidhaa hunyeshwa na Mvua na
mbali na Mvua pia jua ni lao. Katika kutatua changamoto hizo Davis Mosha
aliwaahidi kulifanyia kazi mapema tatizo lao na hatosubiri mpaka muda wa
uchaguzi ufike maana adha hiyo wanayoipata ni wananchi wa Moshi wakiwemo mama
zake na baba zake waliopo hapo Sokoni.
|
Mh. Davis Mosha alipotembelea Soko la Mitumba la Memorial na kujionea changamoto mbalimbali. |
|
Mh. Davis Mosha akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Memoria alipotembelea soko hilo. |
Kutokana na Ahadi hiyo Jana Mh. Mosha aliwasili Sokoni hapo
na Mainjinia kutoka Kampuni ya Group Six ltd
ambao ni Raia wa China kwa lengo la kufanya kufanya vipimo na Michoro
ya uboreahwaji wa Soko hilo ili kuweza kuondoa changamoto zinazowakabili
wafanyabiashara wa Soko hilo. Mainjinia hao walizunguka katika Soko hilo na
kutazama eneo la Soko ili kuweka mipango ya kuanza ujenzi wa Soko hilo ambapo
ujenzi huo hautoathiri wafanyabashara hao kuendelea kufanya biashara zao.
|
Mainjinia
Raia wa China kutoka Kampuni ya Group Six wakiwa soko la Mitumba la
Memorial kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa Matengenezo ya soko hilo. |
|
Mh. Mwigulu Nchemba akimkaribisha Mh. Davis Mosha azungumze na Wafanyabiashara wa Soko la Memorial |
|
Mh. Davis Mosha akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mitumba la Memorial |
Kutokana na utekelezaji huo wa ahadi wananchi mbalimbali
wameonekana kufurahishwa na aina ya kiongozi waliompata ambaye anaomba Ridhaa
ya kuchaguliwa kuongoza Jimbo la Moshi Mjini. Haata hivyo katika mkutano wa
Hadhara uliofanyika jana katika Soko hili ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali
wakiongozwa na Mh. Mwigulu Nchimbi ambaye alipata fursa ya kumzungumzia Davis
Mosha. Mwigulu alisema kazi ngumu kuliko zote ni kutomchagua Davis Mosha kuwa
Mbunge wa Moshi mjini na kazi Rais sana ni kumchagua Davis Mosha. Aliwaambia
wakazi wa Moshi kuwa wana bahati ya kipekee kupata Mbunge ambaye ameanza
utekelezaji wa ahadi zake kabla ya kusubiri bajeti ya serikali na viongozi kama
hao ndi o Tanzania inawahitaji, Kwahiyo ikifika 25 mwezi wa Kumi wasifanye kosa
wamchague Davis Elisa Mosha awe Mbunge wa Moshi Mjini pamoja na Madiwani wake
wa ccm na bila kusahau kumpa kura za Kishindo Mgombea Urais wa ccm Ndugu John
Pombe Magufuli.
Post a Comment