0
Katikati ni mgombea ubunge kupitia CCM, Davis Mosha akiongozana na wazee katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani


Mgombea ubunge jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Mheshimiwa Davis Mosha siku ya jana ameweza kuhudhuria mualiko wa maadhimisho wa siku ya  wazee duniani uliofanyika katika viwanja vya mashujaa moshi mjini.

Maadhimisho hayo yalianza kwa mfumo wa maandamano kutoka maeneo ya posta mpaka viwanja vya mashujaa moshi mjini, ambapo yaliweza kuhudhuriwa na wazee wa mkoa wa Kilimanjaro, viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.

Moja ya sababu ya wazee hawa kuwaalika viongozi wa siasa katika sherehe hizo ni ili waweze kuzungumza nao kuhusiana na matatizo mbalimbali walionayo ili yaweze kupelekwa sehemu maalumu kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

Wazee hao waliweza kuiyomba serikali iweze kuwaanzishia miradi mbalimbali ambayo itaweza kuwapatia kipato, kuwashirikisha katika vikao mbalimbali hasa vile vya kimaendeleo, uwarakishwaji wa pensheni jamii, uboreshwaji wa matibabu, pamoja na kupatiwa vitambulisho vya serikali pasipo kucheleweshwa.

''Sikuja kwa ajili ya kufanya kampeni, nimekuja kwa ajili ya kusikiliza matatizo yenu kama wazee wangu wa Mkoa wa Kilimanjaro hivyo basi nikaona nijitolee gari langu la kipaza sauti ambalo litaweza kusaidia katika maadhimisho yenu pamoja na kusikiliza matatizo yenu" alisema Davis Mosha.

Mosha aliendelea kuzungumza na wazee na kuwaahidi kuwa akichagulia kuwa mbunge wa Moshi Mjini ataweza kuyapeleka matatizo yao sehemu husika ili yaweze kusikilizwa na kufanyiwa kazi.

Hata hivyo mgombe ubunge huyo alendelea kusema kwa kuwa si vyema wazee kujihusisha na siasa hivyo aliona wazee ni kama wazazi wake akaona si vyema aweze kuwa nao sambamba katika maadhimisho yao.

Sio mara ya kwanza maadhimisho haya kuhudhuriwa na viongozi wa kisiasa kwani imekuwa kama utamaduni wa baadhi ya maadhimisho Mkoani Kilimanjaro kuhudhuriwa na wanasiasa.

Wazee wa Mkoa wa Kilimanjaro wakishika mabango yenye ujumbe kwa serikali



Davis Mosha akishuka katika gari lake kuanza maandamano
Wazee wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika maandamano


Davis Mosha akiongea na wazee katika viwanja vya mashujaa







Askari Polisi wakilinda usalama wa wazee katika maandamano yao

















Post a Comment

 
Top